December 15, 2023

LATEST NEWS Death Toll from the Maui fires stands at 93.  

Sydney 29

AFC Leopards wanapanga kuivamia Kakamega Homeboyz na kuwasajili wachezaji watatu, ambao ni Moses Shumah, Brian Eshihanda, na Faruk Shikalo katika dirisha la usajili la katikati mwa msimu,Kwa jumla, Ingwe wanatarajiwa kusajili makipa wawili, mabeki wa kati watano, mabeki wawili wa kulia, mawinga wawili, kiungo wa kati na washambuliaji wawili kwenye dirisha hilo. Wachezaji wengine ambao wanawalenga ni pamoja Brian Mus na Ken Owino wa Posta Rangers, Steve Njung’e, Mark Kwasira na Glen Odhiambo wa Mathare United, Frederick Alushula, Kevin Otiala wote wa Kariobangi South.

Klabu ya Villarreal imevutiwa Na mpango Wa kutaka kumsajili beki Wa kulia Wa arsenal raia wa Ureno Cedric Soares ambaye hayuko kwenye mahesabu ya mkufunzi Mikel Arteta.
Mwalimu Wa spurs Ange Postecoglou amedokeza Kwamba watasajili beki Wa Kati mwezi Januari.

Miamba wa soka nchini Ufaransa PSG, wamemtaja kiungo wa kati Wa Manchester United Na Brazil Carlos Henrique Casemiro kuwa miongoni mwa wale wanataka kuwasajili katika dirisha la uhamisho.

Vilabu viwili katika ligi ya Uingereza Arsenal, pamoja na Tottenham Hotspurs wanapigana vikumbo katika harakati za kutaka sahihi ya kiungo wa royal Antwerp ya Ubelgiji Arthur Vermereen ambaye amekuwa nyota kambini huko.

Mwandishi: Joseph Lewa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *