December 1, 2023

LATEST NEWS Death Toll from the Maui fires stands at 93.  

Sydney 29

Warembo wa timu ya taifa ya Rising starlets walirejea nyumbani siku ya Jumatatu 13, Novemba 2023 kutoka Cameroon. Starlets walichabangwa na wenyeji Cameroon kwa mabao 3-0.

Rising starlets waliondoka Nchini wiki iliyopita kuelekea Cameroon kwa mchuano wa mkondo wa kwanza wa mechi za kufuzu katika kombe la Dunia la wanawake wasiozidi Umri wa miaka 20.

Mpambano huo mkali ulichezwa siku ya Jumamosi, 11 Novemba 2023 saa 7:00 saa za Afrika Mashariki ugani Stade Ahmadou Ahidjo,Yaounde Cameroon.
Kikosi hicho kilichosafiri kilikosa baadhi ya wachezaji muhimu ambao wanaendelea na mtihani wa kidato cha nne unaoendelea, hapo awali Mkufunzi wa Rising starlets Beldine Odemba alieleza wasiwasi wake kutokana na wachezaji hao kutojiunga na kikosi chake.

Kwenye mechi hiyo timu ya Cameroon ilionekana kulemea Starlets katika kipindi cha kwanza ambapo waliweza kufunga mabao yote 3.Kunako dakika ya 19 Annie Engamembem alifunga bao la kwanza na kuongeza lingine katika dakika ya 35 naye Naomi Eto akamaliza udhia zikiwa zimebaki dakika 2 kipindi cha kwanza kikamilike.

Hapo awali Warembo hao walimuondoa Angola kwenye mashindano hayo kwa kumfunga jumla ya 10-1 katika mikondo yote miwili.
Rising Starlets wanatarajiwa kucheza mkondo wa pili dhidi ya Cameroon tarehe 17 mwezi wa Novemba 2023 jijini Nairobi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *