December 1, 2023

LATEST NEWS Death Toll from the Maui fires stands at 93.  

Sydney 29

.

Taasisi ya Smart Applications International imezindua mbinu mpya ya Kimatibabu ya Kidijitali hapa jijini Mombasa ambapo, teknolojia hiyo, itawezesha wagonjwa kupata huduma za Kidijitali.

Akizungumza hapa jijini mombasa, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bwana Harrison Muiru ameeleza kuwa wameshirikisha hospitali zaidi ya Mia Tatu katika Ukanda wa Pwani,huku akisema kuwa Teknolojia hiyo itarahisisha pakubwa kwa kuwahudumia wagonjwa wanaofika katika hospitali hizo ambapo,wataweza kutumia mbinu mpya ya kibayometriki na simu zao za mkononi ili kurahisisha ufikiaji wa huduma za Afya ya Kidijitali kwa Wagonjwa watakao hudhuria huduma za Afya.

Mbali na Huduma hiyo, pia amedokeza kwamba wataweza kujifunza kuhusu Smart Analytics,inayohusiana na maarifa mbali mbali kama vile Biashara na Data ili kuwawezesha kupata huduma ya Matibabu kutoka Kwa Makampuni ya Bima, ambapo wataweza kuleta huduma bora na ufanisi ,vilevile taasisi hiyo inalenga kuelimisha jamii kuhusiana na huduma hiyo mpya ya teknolojia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *